Kocha wa Spurs, Pochettino amemsifia mshambuliaji wake wa muda mrefu, Son Heung-Min kuwa kwa kazi anayoifanya na klabu hiyo hakuna utofauti sana na yale yanayofanywa na Messi hivyo kwake anaona kati ya hao wawili ni sawa tu, hakuna utofauti unaotisha sana kwamba kuna mwingine ana upekee sana. Japo anaona miondoko ya wachezaji hao na uwezo wa kufuata aliko adui yake ni kitu ambacho wawili hao wanacho.
Mchezaji huyo kwa sasa amekuwa akifanya vizuri sana na amekuwa na msimu mzuri sana ndani ya kikosi hicho na kwamba anajaribu kuziba mapungufu ambayo yangejitokeza kutokana na kukosekana kwa Kane na Delle Alli ambao wapo majeruhi kwa sasa. Tangu arudi kutoka kushiriki kombe la timu zinazopatikana ukanda wa bara la Asia amefanya makubwa yanayoibeba timu hiyo iendelee kukaa juu.
Mwalimu wa timu hiyo anaona kuwa hakuna tofauti kati ya hao kutokana na jukumu la kuzisaidia timu zao kupata matokea wakati wa mechi lakini Messi pekee amekuwa akipigiwa upatu juu ya nafasi yake hiyo kwenye kikosi cha timu yao. Kwa wakati huu ambao Spurs inawakosa wachezaji muhimu maana yake kuna uwezekano wa kurudi nyuma au kusonga mbele; lakini mbele ya Son mambo yanaonekana kwenda.
Anarudi kikosini baada ya timu yake ya taifa kutupwa nje ya michuano hiyo na kuwaachia Qatar kombe. Baada ya kumalizika huko, nafasi iliweza kuchukuliwa na Qatar aliye kwenye bara hilo. Na washindani wa muda mrefu wakaishia kumwangalia Qatar akipewa heshima ya kunyanyua kikombe hicho.

Anakwenda kuokoa jahazi la timu hiyo akiwa na magoli yanayomfanya aonekane na upekee wa ajabu kwenye soka.
Son ni aina ya wachezaji ambao wanakufanyia kila kinachowezekana na baadaye wanahitaji kufanyiwa mapumziko ili waweze kupumzika wanapokuwa wamechoka. Anafanya makubwa lakini inapotokea wamechoka kutafuta mpira wanatakiwa kupewa nafasi ya kupumzika na amekuwa kwa misingi hiyo.
Son amekuwa mchezaji anayejituma sana kuifanya timu yao hiyo iendelee kusonga mbele japo hawana bahati ya kunyanyua vikombe katika historia. Ni vigumu kuwafananisha, hili linatokana na sababu iliyopo ya uzuri wa mchezaji au timu anayoichezea lazima uendane na dhima anazopewa na mafanikio ya vikombe; bali sio maelfu ya mechi anazocheza bila vikombe.
Ni vigumu kuwalinganisha wawili hawa kutokana na mafanikio ambayo kwa mmoja mmoja ameyafikia na yanaonekana, labda Son angekua na vikombe ambavyo tayari anavyo mkononi isingekuwa na ubishi wowote kufananisha ubora wao kwa hili. Kufanana kwao ni katika nafasi ya wote kuwa kama wanamichezo; lakini kwenye utofauti kila mmoja ana nafasi yake kikosini juu ya kuipa timu mafanikio.


Povel
Gud news