Bila shaka inaonekana na kufahamika kwamba Klopp sio kocha tu bali ni mwalimu mzuri anayependa wachezaji na anaowaongoza waweze kufanikiwa kwa kuwafua vizuri kwa kuwaamini anapowapa majukumu. Wafuatao ni baadhi ya wachezaji nyota aliowatengeneza na wakadhihirika na ulimwengu kwamba ni bora kwa makubwa waliyoyafanya katika klabu hizo alizoongoza na klabu nyingine duniani:
Robert Lewandowski
Ni suala lisilo na ubishi Klopp amefanya makubwa sana kwenye soka kwa kumtengeneza mchezaji huyu kuwa wa kiwango cha aina yake duniani. Robert ni aina ya washambuliaji hatari sana duniani ambao wanatamaniwa na kila klabu. Alimlea mchezaji huyo na kumkuza tangu wakiwa Dortmund hadi pale alipokuja kumuuza kwa majirani zake Bayern. Akiwa Dortmund alifunga magoli 103 katika mechi 187 alizozicheza uwanjani.
Mats Hummels
Hili ni zao la Bayern ambao walimfunza katika academy yao miaka ya 1995, baadaye wakampeleka kwa mkopo Dorrmund ambako alinolewa vilivyo na Klopp hadi sasa amekuwa hatari sana katika kikosi cha Bayern. Undugu wa klabu hizi mbili ni mkubwa mno na huuziana na kuazimana wachezaji kwa vipindi mbalimbali. Mwaka 2009 alijiunga kuwachezea Dortmund kwa mkataba kabla ya kuja kurudi Bayern akiwa amecheza mechi 309 na Dortmund.
Marco Reus
Majeraha yamemharibu sana mchezaji huyo. Ni chachu sana kwenye soko la mpira wa miguu pamoja na kwamba hajabahatika kucheza mechi nyingi ila amechangia kwa kiwango kikubwa maendeleo ya Dortmund. Shukrani nyingi zimfikie Lucien Favre ambaye alishinda nafasi ya kumuandaa Reus kuwa mchezaji bora duniani. Lakini safari yake haikuishia hapo, alipotua chini ya mikono ya Klopp aliweza kupikwa zaidi na kuwa ni zaidi ya mchezaji.
Philippe Coutinho
Baada ya kutua tu Uingereza alikutana na raia huyo wa Brazil, Coutinho. Aliweza kufanya naye kazi kwa kipindi fulani tu ila aliweza kumtumia ipasavyo na kudhihirisha uimara wake katika kumtengeneza na kumuandaa kwa soko la wachezaji ghali sana kutoka Uingereza.
Ilkay Gundogan
Hadi Man City wakamwona anafaa yalikuwa ni matunda yaliyopandwa na Klopp klabuni pale kwani alikuwa na kikosi ambacho alikitengeneza kwa namma ya pekee sana; na haijawahi kutokea tena kikatokea kikosi alichomiliki Mjerumani huyo.
Hakika anastahili pongezi kwa yote anayoyafanya. Hivyo, Klopp ni mtu hatari sana kwenye soka kuwahi kutokea.

