Kuna Uwezekano Wakaachia Ubingwa...

Makosa wanayoyafanya Liverpool kwenye ligi ya Uingereza kwa sasa ni zaidi ya majuto baada ya kupoteza alama zao muhimu kwenye gemu muhimu ambayo walipaswa kuishinda. Hili limetokea kwa timu hiyo baada ya kutoa suluhu ya 1-1 kitu ambacho kinawapa nafasi kubwa Man City ambao katika hali ya kawaida watafanya kila linalowezekana ili kumpiku Liverpool aliye nafasi ya juu.

Ikumbukwe tu, Liverpool walikuwa mbele ya City kwa jumla ya alama saba lakini kwa sasa zimepungua hadi kufikia alama tatu ambazo ni hatari zaidi na muda wowote wanaweza kupokwa uongozi wa ligi hiyo na wapinzani wao Man City ambao wamejipanga kutaka kuchukua ndoo hiyo kwa mara nyingine.

Sare hiyo ya 1-1 ambayo aliipata katika mechi dhidi ya Leicester, na nyingine aliyoipata juzi mbele ya West Ham United inamfanya awe amepoteza alama nne mkononi hadi sasa ambazo angezichukua hizo zingempeleka mbali sana kwenye ligi hiyo. Pia, katika upande wa pili baada ya City naye kupoteza mbele ya Newcastle kunawapa kiburi zaidi hata Spurs kuweza kuona wanaweza kusogea zaidi kuleta upinzani katika nafasi ya kwanza.

Baadhi ya makosa yanayoweza kuendelea kuwagharimu Liverpool ni pamoja na;

Utoaji mbovu wa pasi. Katika hali halisi klabu hiyo imekuwa ikifanya vizuri katika kutengeneza mashambulizi kwa kucheza pasi nyingi ambazo zinasaidia safu yao ya kushambulia kufanya vyema. Lakini katika nafasi hiyohiyo, wameweza kupoteza pasi za muhimu nyingi sana ambazo kwa namna moja au nyingine zingewapa wao nafasi ya juu zaidi kwenye ligi hiyo.

Katika kipindi cha nyuma kidogo ilionekana Liverpool anafunga sana na alikuwa akifunga magoli mengi katika mechi moja. Lakini mambo yalianza kubadilika kadri siku zinavyokwenda kutoka kutoruhusu magoli kwenye mechi 12, na kwa sasa mambo yamekuwa tofauti wameweza kuruhusu wapinzani kufanya wanachojisikia katika lango lao kwa kiasi kikubwa sana.
Katika kipindi cha nyuma kidogo ilionekana Liverpool anafunga sana na alikuwa akifunga magoli mengi katika mechi moja. Lakini mambo yalianza kubadilika kadri siku zinavyokwenda kutoka kutoruhusu magoli kwenye mechi 12, na kwa sasa mambo yamekuwa tofauti wameweza kuruhusu wapinzani kufanya wanachojisikia katika lango lao kwa kiasi kikubwa sana

Umiliki wa mpira. Pamoja na ubora walionao katika kuhakikisha mpira haupotei hovyo kutokana na kuwa na safu bora ya kiungo na ulinzi lakini suala hili linaonekana kuzoeleka kwa baadhi ya timu na kumwacha afanye anavyotaka lakini wao kutumia nafasi za kushtukiza kutafuta matokeo na kitu hicho kwa asilimia kubwa kimewasaidia sana kuweza kummudu Liverpool; hivyo akifanya marekebisho katika hilo ataona mafanikio.

Uwezo wa kufunga na kuzuia. Katika kipindi cha nyuma kidogo ilionekana Liverpool anafunga sana na alikuwa akifunga magoli mengi katika mechi moja. Lakini mambo yalianza kubadilika kadri siku zinavyokwenda kutoka kutoruhusu magoli kwenye mechi 12, na kwa sasa mambo yamekuwa tofauti wameweza kuruhusu wapinzani kufanya wanachojisikia katika lango lao kwa kiasi kikubwa sana.

Matokeo dhidi ya timu za chini. Amekosa kupata matokeo muhimu kwa timu nyingi ambazo zinaonekana ni ndogo na zenye nafasi ndogo sana ya kufanya vizuri kwenye ligi hiyo. Kufanya hivyo ni kupelekea kupoteza nafasi kubwa ya kuonesha ushindani ndani ya ligi hiyo. Kitu hicho kimewagharimu na kina uwezekano kuendelea kuwagharimu zaidi.

3 Komentara

    Wako vizur sana

    Jibu

    Awawez kiuuachia ubingwa

    Jibu

    Nice

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.