Rasmi : Dean Smith Kocha Mkuu Norwich City.

 

Baada ya tetesi zilizozagaa kwa kipindi cha wiki nzima hatimaye aliyekuwa meneja wa Aston Villa, Dean Smith ameteuliwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Norwich City inayoshiriki Ligi kuu ya EPL.

 

Dean Smith alitimuliwa ndani ya klabu ya Aston Villa wiki moja iliyopita baada ya kupokea vichapo katika mechi 5 mfululizo kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na kocha wa Rangers, Steven Gerrard.

Norwich City inajivunia kumtambulisha Dean Smith kama kocha mkuu mpya” imeandika taarifa katika wavuti ya klabu.

 

“Smith amesaini mkataba wa miaka miwili na nusu na atajiunga Norfolk na kocha msaidizi Craig Shakespeare.” iliongeza taarifa hiyo.

Shakespeare na Smith walikuwa pamoja Aston Villa kabla ya wote kuondoka na sasa kuamua kujiunga pamoja Carrow Road Stadium.

“Zimekuwa siku saba za maajabu, lakini nafurahi sana kurejea na kufanya kazi na Norwich City katika Ligi kuu.

“Ni ukweli kumekuwa na kazi nzuri zilizofanyika ndani ya vilabu hizi ndani ya miaka minne na nusu uliyopita. Na sasa ni kazi yangu na Craig kuendeleza na kuboresha kazi hiyo kwa lengo la kusalia ndani ya Ligi kuu.” alisema Smith.


WIKI NJEMA NA CRAZY TIME CASINO!

Unasababu milioni za kucheza unavyotaka ukiwa na mabingwa meridianbet, lakini unasababu moja ya kushinda mamilioni katika kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo maridhawa wa Crazy Time unakupa sababu hizo kuwa mmoja wa washindi leo hii.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.