Meneja mpya wa klabu ya Newcastle United, Eddie Howe atakosekana kwenye benchi la timu yake leo wanapowakaribisha Brentford baada ya kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona, Covid 19.

Howe amekutwa na Covid-19 ikiwa ni siku yake ya kwanza katika klabu yake mpya baada ya kuchukua nafasi ya Steve Bruce aliyeondolewa baada ya klabu hiyo kununuliwa mwezi uliopita.
Kuelekea mchezo dhidi ya Brentford pale St James Park, msaidizi wake Jason James Tindall na Graeme Jones wanatarajiwa kuongoza timu hiyo leo jioni kuhakikisha wanapata matokeo.
“Nimesikitishwa kwamba sitaweza kuwepo St James Park hapo keshi [leo] lakini ni muhimu kufwata utaratibu na kujitenga.” alisema Howe.
Howe amejitenga hotelini kwa siku 10 na anatarajiwa kukosa mchezo mmoja zaidi dhidi ya Arsenal wikiendi inayokuja.
Unasababu milioni za kucheza unavyotaka ukiwa na mabingwa meridianbet, lakini unasababu moja ya kushinda mamilioni katika kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo maridhawa wa Crazy Time unakupa sababu hizo kuwa mmoja wa washindi leo hii.


