Kane>United, Messi>Barca?

Msimu wa 2021/22 unaendelea kuyoyoma na kama kawaida, mwisho wa msimu ndio, mwanzo wa dirisha la usajili. Harry Kane > Man United, Lionel Messi > FC Barca?

Kwenye dirisha kubwa la usajili lililopita, Kane alikua kwenye rada za kujiunga na Manchester City, Spurs wakakaza mwisho wa siku, nahodha wao akasalia London. Kwa Messi likawa ni picha la kutisha, kwa mara ya kwanza anaondoka Camp Nou na sasa yupo PSG.

Maisha yameendelea, aliyefanikiwa kafanikiwa, aliyetaabika anataabika. Kwenye Ligue 1 msimu huu, Lionel Messi amepachika magoli 2 tu. Mashabiki wa PSG hawana mpango nae, hajazoea kuzomewa uwanjani lakini ndio maisha yake siku hizi kule Parc de Princes.

Kane anafurahia maisha chini ya Antonio Conte lakini, ameweka wazi lengo lake la kutwaa mataji na sio kubeba tuzo za mfungaji bora tu. Ikumbukwe, mshambuliaji huyu hajawahi kutwaa taji lolote akiwa ndani ya jezi ya Spurs. 

United wapo kwenye nafasi kubwa ya kumkosa Erling Haaland ambaye huenda akasajiliwa Real Madrid au Man City. Plan B ni Robert Lewandowski, huenda Bayern wakajikuta wanalazimika kumueka sokoni kutokana na mkataba wake kuwa unaelekea mwishoni na hajaongeza mkataba. Lakini, Lewandowski anamiaka zaidi ya 30, hii ni changamoto kwa United.

Kule Camp Nou, Joan Laporta anafanya mabadiliko makubwa. Swali ni, ilikuwa sahihi kumuachia Messi aondoke kwa sababu za kiuchumi na kisha kufanya usajili mkubwa kama ambavyo wamefanya? Lakini vipi Messi akitaka kurejea nyumbani, Barca watamfungulia milango? Xavi anampango nae? Mfumo wa uchezaji wa sasa utaendana nae? Anataka kulipa alichokifanya CR7 (kurejea Old Trafford)? Kitaeleweka…


SHAOLIN FORTUNES 100 ONJA LADHA YA USHINDI

Maana ya ushindi mkubwa ipo hapa katika mchezo wa SHAOLIN FORTUNES 100 ndani ya kasino maridhawa za meridianbettz. Kwa dau dogo unashinda zaidi, unaweza kucheza mara nyingi uwezavyo huku ukifurahia ladha ya ushindi.

liverpool, Liverpool Kila Mtu Ashinde Mechi Zake., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.