Alexis Sanchez anasema Arsenal ‘itakuwa moyoni mwake daima’ kabla ya mechi yao ya Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Manchester United siku ya Jumapili. Odds kubwa kwenye mechi hii leo Meridianbet.

Vinara wa EPL, ambao wanajivunia faida ya pointi nane dhidi ya Manchester City, wanawakaribisha vijana wa Erik ten Hag katika Uwanja wa Emirates katika mchezo wa mapema Leo Jumapili.
Kabla ya mchezo huo, Arsenal wamekuwa wakirudia kutuma tena baadhi ya mabao yao bora waliyofunga dhidi ya United katika miaka ya hivi karibuni kwenye mitandao yao ya kijamii.
Moja ya mabao hayo ni bao zuri la Sanchez katika ushindi wa 3-0 wa Arsenal dhidi ya United kwenye Uwanja wa Emirates mwaka 2015. Beti na Meridianbet mechi za ligi zote, odds ni kubwa sana, Usikose hii!!.
Na chapisho hilo halikumuacha bila neno Sanchez kwani mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, ambaye aliondoka The Gunners na kujiunga na United mnamo 2018, alisukumwa na uamuzi wa Arsenal kuangazia bao lake. Pata Odds kubwa za soka ukiwa na Meridianbet.
“Umenikumbuka Sitawahi kukusahau pia,” Sanchez aliandika akijibu chapisho la Arsenal kwenye Instagram.
“Utakuwa moyoni mwangu daima. Ulikuwa familia yangu ya kwanza nchini Uingereza.
“Na kila mtu alinitunza vizuri, hasa mashabiki. Kila la heri Gunners.”
Wakati huo huo, Mikel Arteta anasisitiza kwamba wachezaji wake wa Arsenal lazima wawe na sifa za kiakili na kimwili ili kushinda taji la Ligi Kuu msimu huu. Meridianbet wanatoa ODDS kubwa kwenye mechi zote. Bashiri hapa.

“Kuwa na sifa hizo, uwiano huo kwenye kikosi ni muhimu,” alisema Arteta.
“Kuwa na mawazo na uwezo wa kudhibiti hisia zinazohitajika kucheza kwenye jukwaa kubwa ni muhimu sana.
“Kipengele cha kimwili ni muhimu, pia bila hivyo huwezi kushindana kwa zaidi ya miezi 11 katika hali tunazofanyia kazi.
“Hatujawa kwenye mbio za ubingwa kwa miaka mingi. Maneno hayana maana kabisa, tunapaswa kufanya hivyo uwanjani.”

