Beki wa Morocco Nouhaila Benzina aliweka historia katika Kombe la Dunia la Wanawake kwa kuwa mchezaji wa kwanza kuvaa hijab kwenye michuano hiyo. Tembelea duka la ubashiri-Meridianbet kutandika jamvi lako kwa odds kubwa.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 25 alivaa hijabu ya Kiislamu akionekana kwa mara ya kwanza kwenye mashindano hayo.
Nouhaila Benzina
alishiriki katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Korea Kusini, ambao ulikuwa ushindi wa kwanza kwa Morocco kwenye Kombe la Dunia la Wanawake.
Ni moja kati ya timu nane zinazocheza kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya majira ya kiangazi.
Nouhaila Benzina
alikuwa mchezaji wa akiba ambaye hakutumika katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Dunia wa Morocco dhidi ya Ujerumani, ambapo walichapwa mabao 6-0.
Alianza mechi dhidi ya Korea Kusini na mambo yalianza vyema zaidi kwa Morocco.
Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.
Mshambulizi Ibtissam Jraidi alifunga dakika ya sita, likiwa ni bao la kwanza kabisa kwa nchi hiyo kwenye Kombe la Dunia la Wanawake.
Jraidi aliunganisha krosi ya Hanane Ait El Haj na hiyo ilitosha kushinda mechi hiyo. Ukiwa na meridianbet odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti.
Nouhaila Benzina
, ambaye alionyeshwa kadi ya njano wakati wa mechi hiyo, alicheza dakika zote 90.
FIFA iliondoa marufuku ya kuvaa hijab mnamo 2014, na hapo awali iliipiga marufuku kwa miaka wachezaji wa kike kuvalia vazi hilo kwenye mashindano yaliyo chini ya FIFA.
Mashindano ya Kombe la Dunia ya Wanawake wa Vijana wa U-17 mwaka huo yalikuwa mashindano ya kwanza ambapo wachezaji walivaa hijabu za Kiislamu.
Mechi ya mwisho ya hatua ya makundi ya Morocco itakuwa dhidi ya Colombia mnamo Agosti 3. Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.