Pedro Porro Atua Tottenham Kuongeza Nguvu

Pedro Porro anadai kuwa atakosa kuichezea Sporting Lisbon lakini anasisitiza kuwa anafurahia ‘kufuata’ ‘ndoto’ yake ya kucheza EPL baada ya kukubaliana na Tottenham. Odds kubwa za soka unazipata Meridianbet.

 

pedro porro

Pedro Porro alikubali mkataba wa paundi milioni 42 na Spurs Jumatatu jioni na akasafiri hadi uwanja wa ndege wa Luton saa 2.30 asubuhi Jumanne kabla ya kufanyiwa vipimo vya afya na klabu hiyo ya kaskazini mwa London.

Akiongea na wanahabari kwenye uwanja wa ndege, Pedro Porro alisema alighairisha mazoezi na Sporting Lisbon jana kwa kuwa ‘alikuwa amezingatia tu’ uhamisho wake wa Tottenham, lakini akasisitiza kuwa hajachoma daraja lolote na klabu hiyo ya Ureno.

Akizungumza na CMTV kuhusu kuhamia kwake Tottenham, Pedro Porro alisema: “Nina furaha sana kwa hatua hii, lakini pia ninaondoka kwenye klabu ambayo imenipa kila kitu na ninatumai itawaendea vyema.” Ukiwa na meridianbet unaweza kubashiri mubashara, tembelea maduka ya meridianbet uweze kubashiri.

Alipoulizwa kama hamu yake ya kuondoka Sporting Lisbon iliharibu urafiki wake klabuni hapo, Pedro Porro alisema: ‘Nimeacha marafiki wengi hapa. Wanajua tangu nifike nawashukuru sana. Sasa, inabidi nitengeneze maisha yangu, na kufuata ndoto yangu na ninatumai kwamba kila kitu kitaenda vyema.”

Pedro Porro aliendelea kujadili matukio kabla ya uhamisho wake na kama alikataa kufanya mazoezi. Aliwaambia waandishi wa habari: ‘Hapana, hapana Niliuliza tu kama walikuwa wanajadiliana na kichwa changu hakikuwa sawa. Lakini, Sporting pia walielewa vizuri na ninashukuru.”

Porro aliendelea kufichua kuwa bado hajazungumza na meneja wa Tottenham Antonio Conte. Alipoulizwa kama alizungumza na bosi wake mpya, Porro alisema: “Hapana, hapana. Bado.” Beti na Meridianbet mechi za ligi zote, odds ni kubwa sana, Usikose hii!!.

Mkataba kati ya Sporting Lisbon na Tottenham ulionekana kuwa hatarini wakati timu hiyo ya Ureno ilipositisha mazungumzo wiki iliyopita wakati uchunguzi wa kimatibabu ulipowekwa.

Hata hivyo, mazungumzo yalifufuka Jumatatu jioni na bei kupanda kutoka £39m hadi £42m na Sporting wakitaka Spurs kutoa asilimia ya mauzo yao kwa winga Marcus Edwards kama sehemu ya mpango huo.

Tottenham ilikubali masharti hayo mapya na kuomba Porro afanyiwe uchunguzi wa kimatibabu katika klabu hiyo Jumanne asubuhi. Kwa hivyo, kijana huyo wa miaka 23 alikwenda hadi uwanja wa ndege wa Luton saa 2.30 asubuhi.

Iwapo matibabu yake yataendelea kama ilivyopangwa, kuna uwezekano kijana huyo ataweka kalamu kwenye klabu hiyo ya kaskazini mwa London baadaye leo. Meridianbet wanatoa ODDS kubwa kwenye mechi zote. Bashiri hapa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.