Aliyekuwa kocha wa zamani wa PSG, Mauricio Pochettino anataka kazi yake inayofuata ya ukocha iwe na klabu yenye uwezo wa kushinda Ligi ya Mabingwa baada ya uzoefu wake wa kufanya kazi na Kylian Mbappe, Lionel Messi na Neymar katika klabu ya Paris Saint-Germain.

 

Pochettino: "Nataka Timu ya Kubeba Ligi ya Mabingwa"

Pochettino aliondoka PSG mwezi Julai, baada ya kushinda taji la Ligue 1 msimu uliopita huku wakitolewa Ligi ya Mabingwa Ulaya na kushindwa kuchukua taji hilo mwaka uliofuata.

Kocha huyo wa zamani wa Tottenham alishindwa kuifikisha timu katika hatua ya robo fainali licha ya kuwa na kikosi chenye nyota wengi wenye uwezo na kuangushwa na Real Madrid katika mechi ya hatua ya 16 bora.

Pochettino amekuwa hana kazi tangu aondoke PSG licha ya kuwa na ofa nyingi  na sasa ameeleza ni nini hasa anachotafuta katika mradi mpya, na alisema kuwa kuhusu kuzungumza miradi katika soka ni vigumu sana na wachache walio na bahati ambao wanaweza kushiriki katika mradi huu muda ni mfupi au mrefu.

Pochettino: "Nataka Timu ya Kubeba Ligi ya Mabingwa"

Baada ya kuwa katika klabu na Mbappe, Messi, Neymar, ni kawaida kwamba ningetafuta kudumisha kiwango hicho. Klabu ambayo inatoa nafasi ya kulenga makubwa zaidi, kama kushinda Ligi ya Mabingwa itakuwa bora.

Kuhusu Messi, ambaye ana uwezekano wa kushinda Kombe la Dunia akiwa na Argentina huko Qatar 2022 baadaye mwezi huu, Pochettino anahisi kuwa Argentina nao wanweza kutwaa taji hilo msimu huu.

Pochettino alisema kuwa siku zote unaweza kutegemea Argentina lakini pia kuna Brazil na angemjumuisha Uingereza, Ufaransa, Uhispania na Ujerumani.

Pochettino: "Nataka Timu ya Kubeba Ligi ya Mabingwa"

“Argentina inapendelewa zaidi ya miaka minne iliyopita, hasa baada ya kutwaa taji la Copa America. Unapokuwa na Messi, na kila mtu anaelewa ni lazima kumcheza, ndoto zinaweza kutimia.”

Mafanikio kwa Messi yangemfanya amfuate Diego Maradona  mwingine wa nguli wa muda wote wa mchezo huo  katika kuiongoza Argentina kutwaa taji hilo. Maradona na Messi wao ni bora katika mazingira yao.


aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa