Bingwa mara nne wa Olimpiki, Mo Farah, amethibitisha kwamba hatakuwa sehemu ya wanariadha watakaonogesha mbio za mita 5,000 kwenye Michezo ya Olimpiki itakayoandaliwa jijini Tokyo, Japan mnamo 2021.
Farah, 37, aliibuka mshindi wa nishani ya dhahabu katika mbio za mita 5,000 na mita 10,000 kwenye Olimpiki za London 2016 na Rio 2016 kabla ya kuelekeza akili yake kwenye mashindano ya marathon.
Hata hivyo, ameeleza kwamba anataka kutetea ufalme wake kwenye mbio za mita 10,000 nchini Japan.

“Naendelea vizuri na maandalizi, ila nadhani muhimu zaidi ni kuwa makini na mbio moja na kuona ni nini ninachoweza kufanya,” alisema Farah.
Akitangaza marejeo yake kwenye mbio za masafa ya kati, Farah alivunja rekodi ya dunia kwa kukimbia umbali wa mita 21,330 chini ya saa moja kwenye kivumbi cha Diamond League kilichoandaliwa jijini Brussels, Ubelgiji mnamo Septemba 4, 2020.
Baada ya ushindi huo, alitawala Nusu Marathon ya Antrim Coast nchini Ireland ya Kaskazini mnamo Septemba 12 na akakaribia kuvunja rekodi yake mwenyewe kwenye mbio hizo za kilomita 21.
“Bila shaka napata motisha sa. Nina kiu ya kupata mataji zaidi,” akasema kwa kufichua kwamba anapania kuweka rekodi ya kuwa mwanariadha wa kwanza katika historia kuibuka mshindi wa medali ya dhahabu katika mbio za mita 10,000 kwenye Olimpiki tatu mfululizo.

“Itakuwa historia japo tayari nimeweka historia katika mbio mbalimbali ambazo nimeshiriki kwenye riadha hadi kufikia sasa. Kwa mfano, nimekuwa Mwingereza wa kwanza kuibuka mshindi wa dhahabu kwenye Olimpiki mbili mfululizo.”
“Lazima niendelee kufurahia ninachokifanya, nikitabasamu na kuona fahari mafanikio yangu. Japo haya ninayoazimia kufanya ni magumu, naamini kwamba hakuna lisilowezekana,” alisema.
Mnamo Februari 2020, Farah ambaye ni Bingwa mara sita wa dunia, alikashifiwa pakubwa kwa uhusiano wake na aliyekuwa kocha wake Alberto Salazar aliyepigwa marufuku kwa kujihusisha na matumizi ya dawa za kusisimua misuli.
Hata hivyo, Farah alisema kwamba kashfa za aina hiyo ni suala la kawaida katika michezo.
SHINDA NA MERIDIANBET!
Tengeneza pesa kidijitali kwa kubashiri mbio za farasi hapa Meridianbet! Chagua nani ashinde, unakusanya mkwanja.


Elika
Mi Farah Yuko vizur sana
Ernest
Farah atatea vipi ubingwa wakati hatukuwepo?
magdalena
aongeze juhudi za kutosha anaweza shinda
Zeiyana
Kwa uwezo alikua nao mo tutegemee ushindi tu ni bigwa wa olimpiki Mara nne
Tatu
Farah mwariadha makini
Dorophina
Bad news kwa mashabiki wake
Adelta
Mashabiki tunashukuru kwa makala nzuri@meridianbettz
Sauda
Alijitahidi kiasi chake
Mwajumah
Aongeze juhud tu anaweza kushinda#Meridianbettz
Samira
Farah sijui atauteteaje ubingwa wake ilihaki hatokuwepo katika michuano
Saupha mohamed
Apambane
marry
asubir msimu ujao
Caroline
Dahh tulitamani kumuona
Lydia Emmanuel Magoti
Haongeze juhudi wamu nyingine yupo vizuri kiasi chake
Fatina
Safi
Latifa juma mohamed
Alijitahidi kiasi chake
Khadija
Sarah inabid ajitahid kias chake#meridianbettz
Shani
Tutakosa mbio za mo kweny mashindano haya champion wa mita 5000
Nasra
Nice
Mwanahamisi
Safi
Hopemwaikuka
Goo Farah
Fatuma kasomo
Aendelee kujitahidi tu
Janeflora malisa
Good
Gabriel
N habar ya kusikitisha sana kwa Mo Farah kukosa mbio za mita 5000
Christa
Ajipange kwa mbio zijazo
Issa
Tutakosa uhondo wa huyu mtu mita 5000 ndio pake hapa
Sabrina
Daah Farah hatotetea ubingwa wake!
Salma ngende
Asubili msimu hujao
Povel
Farah ajipange msimu ujao bingwa mtetez wa mbio hzo
Rose kapinga
Huyo ndio mo farah
Samiah
Asubiri msimu ujao
Angelina
Angoje msimu ujao
Amiri Kayera
Dah itapooza
felister
Farah atateaje wakati hatokuwepo