Wiki nzima yote hii mechi za ligi kuu ya Italy Seria A ziliendelea na, hapo kesho kutakuwa na mchezo mzuri wa kusisimua ambao ni Milan Derby utakaowakutanisha AC Millan dhidi ya Intermillan.

AC Millan ambao wanaongozwa na kocha mkuu Stephano Pioli ndio mabingwa wapya watetezi wa Serie A msimu uliopita wamecheza michezo minne, wameshinda michezo miwili na wametoa sare mbili huku wakiwa hawajapoteza mchezo wowote na kwenye msimamo wapo nafasi ya 6.

Wakati kwa upande wa Intermillan wakiongozwa na kocha mkuu Simone Inzaghi ndani ya michezo minne wameshinda michezo michezo mitatu na wamepoteza mchezo mmoja na kwenye msimamo wa ligi wapo nafasi ya 3.
AC Millan na Intermillan wanatumia uwanja mmoja kama uwanja wao wa nyumbani wanapocheza na timu pinzani ambapo uwanja huo unajulikana kwa jina la Giuseppe Meazza. Msimu uliopta walipokutana Intermillan alichukua alama nne, nani kuondoka kifua mbele kesho?

