Mchezaji wa Manchester United na timu ya Taifa ya Brazil Antony Santos ameweka rekodi yake ya kwanza kuwa mchezaji wa kwanza kuwafunga goli Arsenal katika kipindi cha kwanza cha mchezo hapo jana katika mchezo wao waliokuwa nyumbani kuwaalika The Gunners.

Antony alitupia nyavuni bao hilo la kuongoza kwa timu yake katika dakika ya 35 ya mchezo ambapo walienda mapumziko ya dakika 45 huku United wakiwa tayari na uongozi wa bao moja kitu ambacho wachezaji wengine hawajaweza kufanya hivyo waliocheza dhidi ya Arsenal msimu huu.
Katika mechi ambazo Arsenal wamecheza na kuruhusu mabao, mabao hayo yalipachikwa katika kipindi cha pili kama mechi dhidi ya Leicester City, Aston Villa na Fulham. Mabao hayo yaliingia kambani kipindi cha pili huku mechi zingine akicheza bila kuruhusu mabao ambapo ni dhidi ya FC Bournemouth, na Crystal Palace pekee.

Antony amejiwekea rekodi hiyo pale Old Traford ambapo alifungua pazia la magoli kwenye mechi hiyo na baadae mabao mengine mawili ya kuipa United alama tatu kufungwa na Rashford huku pia akitoa assist moja hivyo kuhusika na mabao matatu ya United. Huku kwa upande wa Arsenal bao lao likifungwa na Bukayo Saka na mchezo kumalizika kwa mabao 3-1.

