Daniel Ajiunga kwa Mkopo Fulham.

Daniel James sasa ni mali rasmi ya Fulham ambapo ameenda kwa mkopo wa msimu mzima.  Fulham ambayo imepanda ligi kuu ya England msimu huu wamefanya sajili mbalimbali ya wachezaji akiwemo Willian.
Daniel Ajiunga kwa Mkopo Fulham.

Willian Borges ni mchezaji ambaye alishawahi kuwa mchezaji wa Chelsea na Arsenal kabla ya kutimkia katika klabu ya Corinthians ya huko nchini Brazil. Mwalimu wa Fulham anaamini kuwa mchezaji huyo ataenda kuongeza kitu katika kikosi chake kutokana na uzoefu alionao pale ligi kuu ya Uingereza.

Daniel alikuwa ni mchezaji wa zamani wa Manchester United ambapo hakuweza  hakudumu kikosini hapo kwa muda mrefu kutokana na ushindani uliopo kikosini hapo pamoja na kukosa namba hivyo kusababisha ajiunge na Leeds United. Katika timu hiyo pia alipata nafasi japokuwa hakuwa chaguo la kwanza la kocha.

Daniel Ajiunga kwa Mkopo Fulham.

Daniel kwasasa ametolewa kwa mkopo Fulham ambayo inanolewa na kocha mkuu Marco Silva. James ataenda kutafuta changamoto mpya ili  aweze kumshawishi kocha wake wa Leeds Jesse Marsch na hata kocha wa timu hiyo ili awe kwenye kikosi cha kwanza.

Fulham ni moja kati ya timu inayofanya vizuri kati ya zile zilizopanda daraja pale Epl mpaka sasa. Ambapo katika mechi tano walizocheza wameshinda mechi michezo miwili, sare mbili na wamepoteza mchezo mmoja, alama 8 kibindoni huku kwenye msimamo wapo nafasi ya 8 pia.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.