Diaby : Siku Moja Nitarejea PSG.

 

Winga wa Bayer Leverkusen, Moussa Diaby amefunguka na kuweka wazi yupo tayari kurejea katika klabu yake ya zamani ya Paris Saint Germain endapo nafasi hiyo itatokea.

 

Diaby ambaye aliitwa katika kikosi cha Ufaransa mwezi uliopita kuelekea katika michuano ya UEFA National League, aliondoka PSG na kujiunga na Leverkusen mwaka 2019.

“Mimi ni shabiki wa PSG, lakini nilipoondoka ilikuwa nikwaajili ya kupata muda zaidi wa kucheza. Niliiambia nafsi yangu nahitaji kuondoka na kurudi tena nikiwa bora zaidi.” Diaby aliiambia jarida la L’Equipe.

“Kwanini nisirejee PSG siku moja? Moja ya lengo langu ni kurejea kwenye klabu kama hiyo siku moja. Mafanikio katika kazi ni nini? Kuvaa jezi ya timu ya taifa ya ufaransa mara nyingi inavyowezekana, na kucheza katika klabu kubwa. Nikifanikiwa hivyo, haitakuwa mbaya.

“Haya ni malengo yangu kwa sasa. Labda muda mwingine, tukifanya mahojiano, kunaweza kuwa na mengine zaidi.”aliongeza.


SPACE SPIN NA MERIDIANBET.

Ni Mabingwa pekee Meridianbet wanakupa nafasi ya kushinda zaidi na mchezo wa Space Spin katika kasino bomba za meridianbet. Ni wakati wa kufurahia na kutengeza mkwanja bila kuwaza.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.