Kiungo wa Kimataifa wa Kenya, Victor Wanyama ametangaza kustaafu kulitumikia taifa lake akiwa na umri wa miaka 30.

Uamuzi wa wanyama unakuja baada ya kutoitwa tena kwa uteuzi wa kuitumikia Kenya, wakati huu ni mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2022 mapema mwezi huu.
Wanyama, anayechezea CF Montreal ya Ligi Kuu ya Marekani, alionekana mara ya mwisho kuichezea Kenya mnamo Novemba 2020. Alicheza mechi yake ya kwanza mnamo Mei 2007 na alifunga mabao saba katika michezo 64 kwa nchi yake.
Wanyama, mchezaji huyo wa zamani wa Celtic, Southampton na Tottenham Hotspur alikuwa nahodha kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika mnamo 2019, wakati Kenya ilimaliza ya tatu katika kundi lao nyuma ya mabingwa Algeria na Senegal walioshika nafasi ya pili katika mashindano.
Kenya ilishindwa kufuzu kwa Kombe la Mataifa lijalo nchini Cameroon, na ikaachana na kocha Jacob ‘Ghost’ Mulee mwezi huu baada ya kutoka sare mechi zao mbili za kwanza za kufuzu Kombe la Dunia.
Harambee Stars kwa sasa inashika nafasi ya pili katika Kundi E, ikiwa na alama mbili nyuma ya vinara Mali, ambao wana alama nne, na washindi wa kundi pekee ndio wanaotinga hatua ya mchujo ya Afrika kufuzu fainali za Dunia huko Qatar.
SPACE SPIN NA MERIDIANBET.
Ni Mabingwa pekee Meridianbet wanakupa nafasi ya kushinda zaidi na mchezo wa Space Spin katika kasino bomba za meridianbet. Ni wakati wa kufurahia na kutengeza mkwanja bila kuwaza.


