Kocha wa Tottenham aridhishwa na maendeleo licha ya kutolewa Champions League

Kocha wa Tottenham Hotspur, Igor Tudor, amesema ameridhishwa na maendeleo ya timu yake licha ya kuondolewa katika UEFA Champions League baada ya kuchapwa kwa jumla ya mabao 7-5 dhidi ya Atletico Madrid.

Kocha wa Tottenham aridhishwa na maendeleo licha ya kutolewa Champions LeagueTottenham walishinda mabao 3-2 katika mchezo wa marudiano uliopigwa jijini London, lakini matokeo hayo hayakutosha kufuta kipigo cha mabao 5-2 walichopata katika mchezo wa kwanza uliochezwa Hispania chini ya kocha Diego Simeone.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Licha ya kuanza vibaya tangu Tudor achukue mikoba kufuatia kufukuzwa kwa Thomas Frank, Spurs sasa wameanza kuonyesha dalili za kurejea kwenye ubora, wakiwa pia wamepata sare ya 1-1 dhidi ya Liverpool FC mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kocha wa Tottenham aridhishwa na maendeleo licha ya kutolewa Champions LeagueAkizungumza baada ya mchezo huo, Tudor alisema: “Hisia zinachanganyika. Hutaki kutolewa lakini tulicheza vizuri sana. Kulikuwa na hali nzuri uwanjani pamoja na mashabiki waliotuunga mkono tangu mwanzo.”

Aliongeza: “Nawapongeza wachezaji wangu. Kuna mambo mengi mazuri tumeonyesha—jitihada, kasi na nidhamu. Katika mechi mbili zilizopita tumeimarika sana.”

Kocha wa Tottenham aridhishwa na maendeleo licha ya kutolewa Champions LeagueTottenham kwa sasa wako nafasi ya hatari katika msimamo wa Premier League wakiwa pointi moja juu ya eneo la kushuka daraja, huku wakijiandaa na mchezo muhimu dhidi ya Nottingham Forest. Kwa upande mwingine, Atletico Madrid watachuana na FC Barcelona katika robo fainali, huku mshambuliaji Julian Alvarez akikiri kuwa hawakuwa kwenye kiwango bora licha ya kufuzu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.