Jose Mourinho ambaye ni kocha mkuu wa klabu ya AS Roma amesema kuwa hawakuwa na bahati baada ya kupoteza mchezo wao kwa kichapo cha mbwa mwizi hapo jana cha mabao 4-0 ambapo AS Roma walikuwa wageni wa Udinese.

Mourinho alisema kuwa katika timu yake hiyo Paul Dybala ndiye mchezaji aliyecheza vizuri na pia akamsifia mwamuzi wa mchezo huo Fabio Maresca kuwa alichezesha mechi vizuri kwa wenyeji ambapo kwenye mchezo huo Roma alipoteza mchezo huo kwa mabao 4-0, huku hiko kikiwa ndio kipigo chake msimu huu kwenye Serie A.
Licha ya kupoteza mchezo huo Roma walimiliki mpira kwa kiasi kikubwa takribani 56% kuliko Udinese na kuendelea pamoja kupiga mashuti mengi langoni kwa mpinzani na hivyo kusema kuwa makosa waliyofanya katika safu yao ya ulinzi ndio yaliigharimu timu yake kupoteza mchezo huo. Mourinho anasema kwamba,

“Nazungumzia bahati mbaya kwasababu mwanzo tulikuwa tukiimarika kutokana na nafasi aliyopata Dybala, ambaye kwangu alikuwa mchezaji bora zaidi uwanjani.
AS Roma na Mourinho ndani ya Serie A katika mechi tano alizocheza ameshinda mechi tatu, akitoa sare moja na akipoteza mchezo mmoja ambao ni jana akiwa ugenini dhidi ya Udinese huku akiwa katika nafasi ya 5 alama 10.

