Klabu ya Sharjah ya Uarabuni inatarajia kukamilisha usajili wa Pjanic Sharjah kutoka FC Barcelona. Mchezaji huyo ambaye ni raia wa Bosnia anacheza katika nafasi ya kiungo kwenye kikosi chake ana miaka 32.

Miralem Pjanic anaweza kwenda jumanne hii ili kujadili maelezo ya mkataba wake wa miaka mitatu na kisha kusaini kandarasi mpya kama mchezaji mpya wa Sharjah. Mchezaji huyo imekuwa ni ngumu kwake kupata nafasi ya kuanza katika kikosi hicho cha Xhavi Hernandez hivyo ni bora kutafuta changamoto mpya.

Mchezaji huyo anaenda kuitumikia timu hiyo ya Uarabuni ambayo inashiriki Pro League na mpaka sasa imecheza mchezo mmoja na imeshinda mchezo huo. League hiyo ambayo ina timu 14 tu zinazoshiriki league hiyo tu.

