Robertinho Apewa Utawala Simba SC

Robertinho

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa utafanyia kazi mapendekezo ya benchi la ufundi kwenye upande wa usajili ili kuongeza wachezaji imara ndani ya timu hiyo kwa msimu ujao. Tembelea duka la ubashiri-Meridianbet kutandika jamvi lako kwa odds kubwa.

Ni Roberto Oliveira Robertinho, Kocha Mkuu wa Simba amewaomba viongozi wa timu hiyo kuongeza wachezaji wawiliwawili kila idara ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi kwa msimu ujao wa 2023/24 baada ya kushuhudia ubingwa ukienda Yanga.

Kukamilika kwa usajili ndani ya Simba kutamrahisishia Robertinho Oliveira raia wa Brazil kwenye utendaji wake katika kupambania malengo ya Simba. Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

Simba imepishana na mataji yote iliyokuwa inapambania ikiwa ni pamoja na ligi, Azam Sports Federation, Ngao ya Jamii, Kombe la Mapinduzi pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika ikigotea nafasi ya pili kwenye ligi na pointi 73.

Nafasi ya kwanza ni Yanga yenye pointi 78 huku tatu ikiwa kwa Azam FC na namba nne ni Singida Big Stars. Ukiwa na meridianbet unapata odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti.

Salim Abdallah, Mwenyekiti wa Bodi ya Simba amesema wanakwenda kufanya usajili makini na utakaozingatia vigezo vyote ili kuwapa nafasi wachezaji watakaokuja kuonyesha uwezo wao.

Pata odds kubwa kutoka Meridianbet kwa mechi za ligi mbalimbali.

“Kwa namna ambavyo tumefanya kwenye ligi hatujapenda kwani malengo yetu hayajafikiwa hivyo ambacho tunakifanya ni kufanyia kazi makosa yaliyopita na kufanya usajili mzuri kwenye kila idara.

“Kikubwa ambacho tunahitaji kwa msimu ujao ni kuwa tofauti na kupata kile ambacho tunahitaji. Usajili wetu ujao tunaamini utakuwa mzuri na tunaamini kila kitu kitakuwa sawa kwani tunaendelea vizuri,”.

Acha ujumbe