Kulingana na ripoti kutoka Ureno, wamiliki wa zamani wa Inter, Suning wako mbioni kuwekeza euro milioni 80 kununua klabu ya Portimonense.

Tovuti ya ZeroZero inadai kuwa chanzo kilicho karibu na mazungumzo hayo kilithibitisha kuwa makubaliano hayo yapo tayari kuingia katika hatua muhimu.
Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.
Inaonekana itajumuisha ununuzi wa uwanja wa michezo wa Portimao na kituo cha mafunzo cha timu ya Vijana chini ya miaka 23.

Kwa sasa Portimonense inashiriki ligi ya daraja la pili ya Ureno, kwani ilishuka daraja mwishoni mwa msimu uliopita, na kumaliza katika nafasi ya 16 kati ya timu 18.
Hii itakuwa ni kurejea haraka katika ulimwengu wa soka kwa Suning, kampuni ya China inayoendeshwa na familia ya Zhang ambayo ilikuwa inaisimamia Inter kutoka 2016 hadi 2024.


