Klabu ya Azam FC leo itakuwa ugenini kucheza dhidi ya Ihefu katika mwendelezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara ambapo mchezo huo utapigwa katika uwanja wa Highland Estate Mbarali majira ya saa 10:00 jioni.
Azam FC ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi baada ya kushinda mechi zake 14, kwenye michezo yake 24 ambayo ameshacheza, akishinda michezo mitano na kupoteza mitano pia.
Vijana wa Kally Ongala wakipata ushindi hii leo watapanda hadi nafasi ya tatu ambayo kwasasa anashikilia Singida Big Stars aliyetoka kutoa sare jana akiwa na pointi zake 48 hadi sasa.
Ihefu wao ambao ndio wenyeji wa mchezo wapo nafasi ya 8, kwenye michezo 24 wameshinda michezo tisa, wakienda sare mara tatu na wamepoteza michezo yao 12, wakivuna pointi zao 30.
Ushindi wa leo utawafanya Ihefu wapande hadi nafasi ya sita kutoka ya nane, hivyo timu zinazoenda kukutana leo kila timu inahitaji ushindi wa hali na mali aweze kusogea kwenye nafasi inayofuata.
Mechi ya mwisho kukutana Azam alionodk ana ushindi. Je ni nafasi ya Ihefu na wao kupata ushindi leo? ODDS KUBWA unazipata mechi hii.