CAF Yawapeleka Simba Kenya

simba

KWA mujibu wa taarifa za ndani zimeeleza kuwa kikosi cha Simba SC kinatarajia kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wa Ligi ya mabingwa wa Afrika dhidi ya Power Dynamos nchini Kenya. Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

Mtoa taarifa hizo aliweka wazi kuwa kama safari yao itakubali na itakapokuwa nchini Kenya huenda ikacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya nchini humo.

Simba wameanza kujiandaa na mchezo wa mkondo wa kwanza dhidi ya Power Dynamos utakaopigwa jumamosi ya Sept 16 kwenye mji wa Ndola, Zambia kwenye Uwanja wa Lavy Mwanawasa, uliopo kwenye Barabara Kuu ya Kitwe.

Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.

Lakini chanzo hicho kilidokeza zaidi kwamba wakiwa Kenya wanaweza kucheza michezo miwili hadi mitatu ya kirafiki wakiwa na kisha wakafanya safari kutoka Kenya hadi Ndola kwa ajili ya mchezo.

“Timu inakwenda Kenya kwa mipango ambayo ipo kwa ajili ya maandalizi ya Ligi ya Mabingwa Afrika Lakini pia ni sehemu ya kujiandaa na mashindano mapya ya African Super League,” alisema.

Kwa upande wa Ahmed Ally alipotafutwa alisema wazi kuwa: “Nafikiri wewe na Watanzania wote wanajua kuwa Simba haina mzaha awamu hii kwenye mashindano ya Caf, wapi tutaweka kambi na wapi tutakaa hiyo inabaki kuwa kwenye mipango ya kutoboa kimataifa.”

Ukiwa na meridianbet odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti.

Acha ujumbe