Chimbuko la Vipaji laibua kina Mandonga wapya, huku wachezaji 137 washiriki jumla ya fainali 14 kupigwa Tandale jijini Dar es salaam.
Fainali za Mashindano ya Taifa ya Ubingwa wa Wazi 2023 kufanyika leo katika Ukumbi wa CCM Manyara Park, Tandale.
Jumla ya mapambano 14 katika kila uzani yatafanyika kuanzia majira ya saa 9 alasiri na mgeni rasmi atakua Ndugu Wilfred Nyamwija, Mkurugenzi wa kampuni ya Dinari Investments na Diwani wa Kata ya Hananasif.
Mashindano haya yalianza rasmi siku ya Jumanne 31-05-2023 ambapo jumla ya wachezaji 137 kutoka vilabu 19 walijiandikisha kushiriki.
BFT imeamua kuwafuata mabondia mtaani ili kuibua vipaji vipya na imejiidhirisha baada ya kuibuka majina mapya na kufika hatua za fainali kama vile Victor Njile (Morogoro), Shuku (Kyela) na Kelvin “Ngosha” (Iringa)
Mwaka jana mashindano haya yalifanyika katika uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Pamoja na mashindano haya Shirikisho limeendesha mafunzo ya ngazi ya Taifa Daraja la 1 na la 2 kwa Walimu na Waamuzi na Majaji (R&J)