Taarifa kutoka Afrika kusini Zimethibitisha kuwa Klab ya Kaizer Chiefs nayo imeingia kwenye Mbio za kuiwania saini ya Winga Luis Miquissone.
Hapo awali ilifahamika kuwa Luis Miquessone atajiunga na Simba na Makubalino binafsi yalikwisha fikiwa tayari.
Sasa klabu ya Kaizer Chiefs inadaiwa kuingilia Usajili huo huku wakimpa ofa nzuri ya ada Usajili na hata Mshahara wake.
Kwasasa Mchezaji huyo wa kimataifa wa Msumbiji Luís Miquissone anafanya mazoezi katika uwanja wa Desportivo do Tchumene Sport Complex nchini Msumbiji akijiweka fiti huku akisubiri kuamua kuhusu hatma ya klab yake Mpya anayohitaji kwenda.
Kama ni Simba Sc ama Kaizer Chiefs Licha ya kuwa Luis Miquessone Mwenyewe Mapenzi yake yapo Simba ila Wakala wake ndiye anayechelewesha winga huyo kujiunga na klab hiyo ya Simba (Mara nyingi mawakala huangalia pesa zaidi).

