Winga wa Azam FC Kipre Jr amekuwa na kiwango kizuri sana kwa msimu 2023/24, unaweza kusema moja kati ya waliochangia kwa kiasi kikubwa klabu hiyo Kumaliza hatua ya pili, na kushiriki klabu bingwa Afrika, kwa msimu ujao wa 2024/25. Jisajili Meridianbet kwa ushindi mkubwa wa mamilioni, cheza pia kasino ya mtandaoni.
Utawala mpya umesimikwa ndani ya Ligi Kuu Bara huku Klabu ya Azam FC ikiwa ni miongoni mwa timu ambazo zimefanya kweli kweye ushindani.
Wakati wakiwa na mchezaji namba mbili kwenye chati ya ufungaji ambaye ni Feisal Salum akiwa katupia mabao 19 na pasi saba za mabao kuna mwamba anaongoza kwa pasi za mwisho.
Ipo wazi kwamba namba moja kwa utupiaji ni Aziz KI kutoka Yanga ametupia mabao 21 na pasi nane za mabao akihusika kwenye mabao 28 kati ya 71 yaliyofungwa na mabingwa hao wa ligi.
Anaitwa Kipre Jr nyota wa Azam FC anajua kufunga na kutoa pasi yeye ni namba moja kwa wakali wa kutengeneza pasi za mwisho ndani ya ligi.
Nyota huyo chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Yusuph Dabo ametengeneza pasi 9 za mabao msimu wa 2023/24.
Azam FC ni namba mbili kwenye msimamo ikiwa na pointi 69 safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 63. Meridianbet inakuzawadia promosheni kibao za kasino ya mtandaoni, jiunge na familia hii ya mabingwa kufurahia mgao wa mamilioni.