Baada ya kupoteza mechi iliyopita dhidi ya Yanga, KMC wakuwa ugenini hapo kesho kuvaaana na Kagera Sugar katika mchezo wao wa 10 huku Wanankurukumbi nao wakitoka kupoteza mechi yao ya mwisho.

KMC kabla ya kupoteza mechi ya mwisho walikuwa na mwenendo mzuri ambapo waliweza kumfunga Azam, Sare dhidi ya Simba lakini pia waliweza hadi kusogea katika nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi kuu ya NBC.
Kagera wao hali yao ikiwa ni mbaya baada ya kupoteza mchezo uliopita, waliamua kumfukuza kocha wao na jana kumrejesha aliyekuwa kocha wao Mecky Mexime ambae alidumu na kikosi hicho kwa muda.

KMC yupo nafasi ya 8 baada ya kucheza michezo 9 ushindi mara 3 sare 4 na kupoteza michezo miwili na pointi zao 13. Wakati Kagera wao wapo nafasi ya 13 wakiwa wameshinda mechi 2 baada ya michezo 9, sare mbili, kupoteza mara 5, na pointi 8 tu.
Mechi 5 za mwisho kukutana hizi timu vijana wa Thiery Hitimana wameshinda mara moja, Kagera mara mbili na wameenda sare michezo miwili. Hivyo Wanankurukumbi watakuwa na kocha mpya hapo kesho uwanjani.


