Torres Kutua Arsenal Januari

Arsenal wanafikiria kumnunua Facundo Torres kutoka klabu ya Orlando City, kwa mujibu wa ripoti. Meneja Mikel Arteta, ambaye kwa sasa timu yake ipo kileleni mwa Ligi Kuu kwa tofauti ya pointi mbili, anatazamia kuongeza nguvu zaidi kwenye kikosi chake huku wakipania kuendeleza mbio za ubingwa msimu huu, na anataka kuongeza winga wa upande wa kulia kwenye safu yake ili kuleta ushindani, kwa Bukayo Saka.

 

Torres Kutua Arsenal Januari

Arsenal wanatazamiwa kufanya mazungumzo na raia huyo wa Uruguay na mawakala wake baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kuonyesha kiwango kizuri katika msimu wa MLS wa 2022 akiwa na Orlando City.

Torres alifunga mabao tisa na kusaidia mabao 10 katika mwaka wake wa kwanza katika klabu hiyo baada ya kujiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka minne kutoka Penarol mwezi Januari kwa takriban paundi milioni 7.75.

Inasemekana kwa sasa haijafahamika iwapo Arsenal watafutilia mbali uhamisho huo baada ya mazungumzo ya awali, lakini mazungumzo yataanza hivi karibuni.

 

Torres Kutua Arsenal Januari

Lima ni mtaalamu wa vipaji vya Amerika Kusini na anasifiwa kuwa mmoja wa watu wa kwanza kuwaona Neymar na Philippe Coutinho wakati wa kucheza kwao Brazil.

Arsenal pia wamehusishwa na Pedro Neto wa Wolves na Mykhaylo Mudryk wa Shakhtar Donetsk, lakini inaaminika Torres ndiye kinara wa orodha ya walengwa, huku ikionekana uwezekano mkubwa wa winga kuwasili Januari.

Acha ujumbe