KIUNGO wa Yanga mzaliwa wa Zanzibar Feisal Salumu Abdallah (Feitoto) amefichua kuwa wakati anaingia uwanjani siku ya Jumatano na kufunga bao la ushindi kwa Yanga dhidi ya KMC alitoka kuugua tumbo.

Fei alisema, wakati anafanya maandalizi ya mwisho kuingia kwenye mechi hiyo alianza kuhisi kupata maumivu ya tumbo na hapo akawa ameshindwa kuanza mchezo huo, ingawa tayari alikuwa yupo kwenye mipango ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza.

Feitoto, Feitoto Aliwafunga KMC Akiwa Mgonjwa, Meridianbet

Akizungumza baada ya mchezo huo kumalizika Fei alisema: “Wakati nakaribia kwenda uwanjani, bahati mbaya nikaanza kusikia maumivu ya tumbo. Ndipo ikabidi kocha anipumzishe lakini nilikuwa naanza kwenye kikosi cha kwanza.

“Nashukuru Mungu baada ya kuingia kwenye mchezo ule nikawa nimefuata maelekezo ya kocha ni nikafanikiwa kuipa ushindi na alama tatu kwa timu yangu na ndiyo tulichokuwa tunakihitaji.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa