Sadio Kanoute, kiungo mgumu ndani ya kikosi cha Simba hali yake inazidi kutengemaa mdogomdogo baada ya kuugua ghalfa kabla ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga.

Nyota huyo raia wa Mali hakuwa sehemu ya mchezo dhidi ya Yanga uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Oktoba 23 na kukamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1 kutokana na kutokuwa fiti.

KANOUTE, KANOUTE MAMBO SAFI SIMBA, Meridianbet

Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda alisema kuwa kwa sasa maendeleo ya mchezaji huyo yanaendelea vizuri akiwa chini ya uangalizi wa madaktari.

“Nilisema kwamba kabla ya mchezo kuwa tuwaombee wachezaji wetu kwani ni binadamu, ilikuwa hivyo Kanoute alikuwa mzima ila ghafla alipatwa maumivu kwenye mwili na hali yake haikuwa nzuri.

“Kwa sasa tunamshukuru Mungu anaendelea vizuri hivyo tuzidi kuwaombea wachezaji wetu warejee kwenye ubora wao kwani tumekosa pia huduma ya Shomari Kapombe na Jimson Mwanuke ambao nao taratibu wanazidi kuimarika,” alisema Mgunda.

Pia kwenye mchezo wa Simba dhidi ya Azam FC uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa,  Oktoba 27 hawakuwepo.


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa