Kanoute : Ligi ya Tanzania (TPL) ni Ngumu.

 

Kiungo mkabaji wa Simba SC, Sadio Kanoute, amekiri Ligi Kuu ya Tanzania (TPL) ni ngumu kutokana na timu nyingi kucheza soka lenye matumizi makubwa ya nguvu.

 

Kanoute amezitazama mechi zetu mbili za ligi dhidi ya Biashara United na Dodoma Jiji na kusema matumizi ya nguvu ni makubwa hivyo si rahisi na inapaswa kujipanga vizuri ili kuimudu.

Kiungo huyo ameongeza kuwa changamoto nyingine aliyoiona kwenye ligi ni aina ya viwanja vinavyotumika hasa eneo la kuchezea (pitch) si rafiki na wakati mwingine timu ilazimika kubadili mfumo ili kuendana na mazingira.

“Nimepata nafasi ya kuziangalia mechi zetu za kwanza, kiukweli ligi ni ngumu sababu timu nyingi zinatumia nguvu kubwa na viwanja navyo si rafiki sana lakini tunapaswa kuyakabili mazingira,” amesema Kanoute akinukuliwa katika tovuti ya klabu.

Kanoute amerejea mazoezini jana baada ya kupona maumivu ya bega aliyopata katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga SC uliopigwa Septemba 25, Uwanja wa Benjamin Mkapa.


SPACE SPIN NA MERIDIANBET.

Ni Mabingwa pekee Meridianbet wanakupa nafasi ya kushinda zaidi na mchezo wa Space Spin katika kasino bomba za meridianbet. Ni wakati wa kufurahia na kutengeza mkwanja bila kuwaza.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.