Mbappe : PSG Wamenikosea, Nilitaka Kuondoka.

 

Mshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappe ameilaumu klabu hiyo kwa jinsi walivyoshughulikia uhamisho wake kufeli kwenda Real Madrid na kusisitiza kuwa aliifahamisha klabu hiyo ya Ufaransa juu ya hamu yake ya kuondoka mwezi Julai.

 

Akiongea na kituo cha redio cha Ufaransa RMC Sport, Mbappe amesema: “Nilitaka kuondoka, Kwa sababu wakati huo kwamba sikutaka kuongeza kandarasi yangu nilitaka klabu ipate na ada ya uhamisho mapema ili kupata mbadala mwingine ubora.

PSG ni klabu ambayo imeniletea mengi. Nimekuwa na furaha kila wakati, miaka minne ambayo nimetumia hapa, na bado niko. Nilitaka kila mmoja atoke kwa faida hii, kwamba tuachane mkono kwa mkono, kufanya makubaliano mazuri na niliheshimu hilo; Niwaambia ikiwa hamtaki niende nitabaki.

“Watu wamesema kwamba nilikataa ofa sita au saba za kuongeza mkataba, kwamba sitaki kuzungumza na mkurugenzi wa michezo, Leonardo, hii sio kweli kabisa”.

Mbappe, ambaye ameshinda mataji matatu ya Ligue 1 na matatu ya Kombe la Ufaransa, ndiye mfungaji bora wa PSG msimu huu akiwa na mabao manne kwa kikosi cha Mauricio Pochettino.


SPACE SPIN NA MERIDIANBET.

Ni Mabingwa pekee Meridianbet wanakupa nafasi ya kushinda zaidi na mchezo wa Space Spin katika kasino bomba za meridianbet. Ni wakati wa kufurahia na kutengeza mkwanja bila kuwaza.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

Acha ujumbe