Kiungo wa zamani wa klabu ya Yanga Saidoo Ntibazonkiza anayecheza Geita Gold FC Saidoo Ntibazonkiza amefunguka kuwa mechi yao ijayo ya Yanga kwake anaitazama kwa umakini mkubwa.

Saidoo ambaye alifunga bao moja na kutoa pasi ya bao kwenye ushindi wa 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting juzi Jumatano alisema kila mechi kwake atakuwa anaicheza kama fainali na hata kwenye mchezo wao ujao na Yanga atacheza kwa hali ile ile.

Yanga, Saidoo Awataja Yanga Huko, Meridianbet

Akizungumzia mchezo huo unaotarajiwa kupigwa kesho kutwa Jumamosi kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza alisema: “Kwangu kila mchezo naucheza kama fainali. Siyo mimi tu, bali kila mchezaji kwenye timu yetu anacheza kwa moyo huo.

“Ndiyo Yanga ni timu kubwa na siwezi kusema neno linguine tofauti na kwenda kujituma zaidi na kuweza kuisaidia timu yangu kupata alama tatu muhimu. Hayo ndiyo malengo yangu pamoja na timu.”

Sadoo aliondoka kwa mazingira yasiyotarajiwa na wengi mwishoni mwa msimu uliopita kwa madai ya awali ya kuwa ni mtovu wa nidhamu na kisha baadae ikaja taarifa kuwa ameondoka kwenye klabu hiyo kwa makubaliano ya pande zote mbili.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa