LIVERPOOL YAENDELEA KUKAA KILELENI

Klabu ya Liverpool imeendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kupata matokeo ya ushindi leo dhidi ya klabu ya Crystal Palace wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani.

Liverpool wakiwa ugenini katika dimba la Selhurst Park wamepata ushindi mwembamba wa goli moja ambao umewafanya waendelee kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Uingereza, Mchezo ambao ulionekana kua mgumu licha ya majogoo kuutawala kwa kipindi kirefu.liverpoolDiogo Jota ndio mchezaji aliyefunga goli pekee lililowapa alama tatu majogoo wa Anfield katika mchezo huo ambao wenyeji klabu ya Crystal Palace walionekana kuzuia kwa umakini mkubwa katika boksi lao, Huku wakifanya mashambulizi ya kushtukiza katika lango la vijana wa Arne Sloti japo hawakufanikiwa kupata  goli.

Klabu ya Liverpool baada ya kucheza michezo 7 ya ligi kuu ya Uingereza wamefanikiwa kukusanya alama 18 wakishinda michezo sita, Huku wakifungwa mchezo mmoja tu mpaka sasa na wakiwa hawajasuluhu mchezo wowote hali iliyowafanya kuendelea kusalia kwenye kilele cha msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.

Acha ujumbe