Golikipa wa klabu ya Liverpool Allison Becker ameripotiwa kupata majeraha ya misuli ambayo yalimfanya kushinda kumalizia mchezo wa klabu yake dhidi ya klabu ya Crystal Palace mchana wa leo.
Golikipa huyo alishindwa kumaliza mchezo baada ya kupata maumivu ya msuli wa paja na kutolewa nje na kuingia golikipa namba mbili wa timu hiyo, Hii sasa inakua kama tatizo la kudumu kwa golikipa huyo ambapo amekua akisumbuliwa na majeraha mara kwa mara siku za hivi karibuni.Golikipa Allison Becker bado haijafahamika majeraha hayo ya msuli wa paja yatamueka nje kwa muda gani lakini mpaka sasa ni kua golikipa huyo raia wa kimataifa wa kibrazil anasubiri kufanyiwa vipimo na timu ya madaktari wa klabu hiyo ili waweze kutambua ukubwa wa jeraha.