Golikipa wa klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya Brazil Allison Becker inaelezwa bado yupo sana katika viunga vya Anfield licha ya tetesi mbalimbali zinazoendelea kumuhusu kwasasa.
Allison Becker siku za hivi karibuni amekua akihusishwa na kujiunga na vilabu vya Saudia Arabia, Lakini taarifa zinaeleza kua klabu hiyo haina mpango wa kumuachia golikipa huyo namba moja wa klabu hiyo.Kumekua na ofa kutoka vilabu kadhaa vya Saudia kwenda kwa golikipa huyo wa kimataifa wa Brazil tangu mwezi Machi mwaka huu, Lakini kipaumbele cha golikipa huyo ni kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake jijini Liverpool.
Golikipa huyo amekua mhimili ndani ya klabu ya Liverpool kwa muda mrefu sasa hivo sio rahisi kwa klabu hiyo kukubali kumuachia kwa wepesi, Kwani hata umri wake bado unaruhusu bado kucheza kucheza kwenye kiwango cha juu.Mpaka sasa klabu ya Liverpool na golikipa Allison Becker wote wanaongea lugha moja kwani mpaka sasa klabu hiyo kipaumbele chake ni kumbakiza golikipa huyo klabuni, Lakini pia golikipa huyo mipango yake ni kuendelea kusalia ndani ya viunga vya Anfield kwa misimu mingine mbele.