Alisson Becker:Tunapaswa Kuongeza Ubora

Alisson Becker alikiri hitaji la Liverpool kuongeza uthabiti na uboreshaji katika uchezaji wao kwenye michezo inayofuata.

Liverpool walinyimwa ushindi wa tatu mfululizo wa Ligi kuu na majirani zao Everton Jumamosi, huku mechi ya 241 ya Merseyside derby ikiisha bila bao.

Alisson Becker:Tunapaswa Kuongeza Ubora

Licha ya matokeo hayo lakini, pambano hilo lilikuwa na mfululizo wa nafasi huku wenyeji wakigongesha nguzo na kufunga bao lililokataliwa, kwa upande wa Majogoo walizimwa michomo yao mara tatu na Jordan Pickford.

Alisson alihisi kuonyesha kwa Liverpool kujengwa juu ya ushindi uliotangulia dhidi ya AFC Bournemouth na Newcastle United lakini akaashiria maendeleo zaidi ambayo yatahitajika kutoka kwa vijana wa Jürgen Klopp.

Alipoulizwa kama Liverpool walifanya vya kutosha kushinda dabi hiyo, kipa, ambaye aliokoa michomo ya Neal Maupay na Dwight McNeil katika dimba la Goodison Park, aliiambia Liverpoolfc.com: “Hatukushinda kwa hivyo jibu ni hapana.

Alisson Becker:Tunapaswa Kuongeza Ubora

“Lakini tulifanya vizuri, tuliboresha uchezaji wetu katika mechi za mwisho, tulitengeneza nafasi, nafasi nyingi za wazi. Tungeweza kufunga lakini wapinzani pia walipata nafasi zao. Alisema Allison

Pia Alisson aliongeza kuwa wanajilinda vizuri, kiasi cha kuweka lango safi “clean sheet“, hilo ni lengo la kawaida kwao, wanafanya kazi kwa bidii, baada ya kupata alama moja ugenini wanapaswa kusonga mbele.

Alisson Becker:Tunapaswa Kuongeza Ubora

Liverpool sasa wataelekeza mawazo yao kwenye mwanzo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa, na safari ya kwenda Napoli kwanza kwenye ratiba yao wiki ijayo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.