Kocha mkuu wa klabu ya Barcelona Xhavi Hernandez amesema kuwa suala la wao kushinda mchezo dhidi ya Sevilla ni ishara nzuri kwao ambapo jana walikuwa ugenini kukipiga dhidi ya Sevilla na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.
Raphina ndiye alifungua pazia la kufunga katika mchezo wa jana na baadae Robert Lewandowiski nae akaingia nyavuni ambapo alifunga bao lake la tano katika Laliga. Miamba hao wa Catalunya wamefunga mabao matatu katika mechi tatu za msimu huu, Barcelona wanaonekana kwenye sura mpya, huku wakiwa na ubora mwingi msimu huu. Xhavi anasema kuwa,
“Tumekuwa tukitengeneza nafasi nyingi za kufunga mabao zaidi. Ni ishara nzuri kuja kwa Sevilla na kujituma”. Timu ipo katika wakati mzuri sana.
Xhavi na vijana wake katika Laliga wapo nafasi ya pili kataika msimamo baada ya mechi nne walizpocheza huku wakishinda tatu, sare moja na alama zao 10 ambapo wameachana na Real Madrid alama mbili tu ambapo Madrid ana alama 12.