Klabu ya Barcelona imefikia makubaliano ya kusitisha mktana na mchezaji wa kimataifa kutoka Denmark Martin Braithwaite baada ya mavituno ya miezi kadhaa kutokana na swala kupunguza mshahara wake.

Martin Braithwaite tokea klabu ya Barcelona ifanye maingizo mapya kwenye klabu hiyo kama, Pierre-Emerick Aubameyang na Robert Lewandowski amekuwa na nafasi finyu kwenye kikosi hicho na kupelekea kufikia makubalino ya kusitisha mkataba wake, japo mkataba na klabu hiyo ulikuwa unafikia tamati mwaka 2024.

Barcelona, Barcelona Wavunja Mkataba na Martin Braithwaite, Meridianbet

 

Martin Braithwaite alijiunga na klabu ya Barcelona mwaka 2020 kwenye majira ya baridi, kwenye miaka miwili aliyoitumikia klabu hiyo amefanikiwa kucheza jumla ya michezo 58 ma kufunga magoli 10 na kusaidia kupatika magoli sita kwenye mashindano yote.

Braithwaite mpaka sasa tayari ameshepojea offa kutoka klabu ya Espanyol na anatarajia  kujiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu na uhamisho huo unaweza kukamilika ndani ya saa chache zijazo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa