Barcelona: Tutamuuza Martin Braithwaite

Ni mwezi mmoja tu tangu mshambuliaji wa klabu ya Barcelona Martin Braithwaite kujiunga na timu hiyo, na yawezekana ikawa ndio mwisho wake wa kutumikia Barcelona kutokana na  hali ya ukata uliyoikumba timu hiyo kiasi cha kukaa mezani na kujadili na wachezaji wake juu ya kupunguza mishahara yao kwa zaidi ya asilimia Hamsini.

Magwiji hao wa soka duniani wanatarajia kumuuza mshambuliaji  huyo wa zamani wa timu inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza, Middlesbrough na baadae kujiunga Leganes ya Uhispania kabla ya kutimkia Barcelona. Licha ya kusaini kandarasi ya miaka minne na timu ya Barcelona ambayo ilipaswa kuisha mwaka 2024, muda wake katika timu hiyo utakua umekwisha baada ya kucheza mechi tatu pekee kwenye ligi kuu ya Uhispania maarufu kama La Liga.

Martin Braithwaite

Vyanzo vya habari nchini Hispania vinasema Barca hawataruhusu mchezaji  huyo mwenye asili  ya Denmark  kutoka bila ada ya Pauni milioni 16.1, na imethibitika kua vilabu vya Uingereza kama Everton na West Ham wanatarajia kumrudisha mshambuliaji huyo katika ligi kuu ya Uingereza

Braithwaite hakufanikiwa kufumania nyavu katika mechi zake zote tatu alizotumikia Barcelona, Lakini ameonesha mchango mkubwa sana kwa wachezaji wenzake na timu kiujumla. Ameeleza kuwa anaamini uhamisho huo unaweza kubadilishwa na kuna uwezekano wa yeye kurudi tena Barcelona kipindi cha majira ya joto.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.