Wito wa Bondia Anthony Yarde kwa Umma

Mwanandondi Anthony Yarde ametoa wito kwa watu kusalia majumbani kufyatia janga lilomfika baba yake. Wakati ulimwengu ukiwa unapambana vilivyo kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona, haikuwa bahati kwa babaye Anthony Yarde. Anthony ameweka wazi kuwa baba yake amefariki kwa sababu ya kupata maambukizi.

Bondia huyu ametoa taarifa hii kwa uchungu akiwa na kusisitiza umuhimu wa kusalia nyumbani. Bodi ya Michezo ya Ndondi BBBC iliamua kuahirisha mapambano yote yaliyokuwa yafanyike kipindi hiki hadi pale mwishoni mwa mwezi April katika kuunga mkono uepukaji wa misongamano na kujitenga ili kuzuia maambukizi ya Corona.

Yarde ametoa taarifa hizi za huzuni kupitia ukurasa wake wa Instagram huku chapisho lake likisomeka:

“Mimi ni mtu wa kutojiweka hadharani sana, lakini nikiwa muwazi kabisa, bado nipo kwenye mshtuko lakini nafikiri hii itawasaidia watu kusali majumbani kwao. Baba yangu amefariki kutokana na hivi virusi jana na alikuwa safi bila shida yeyote ya afya. Kadri watu wanavyotoka nje na kuonana ndivyo kujitenga hivi kutakavyo chelewa kuisha na maambukizi kushika kasi zaidi. Mimi sio daktari lakini nafahamu ukisalia nyumbani unakuwa kwenye hatari ndogo zaidi ya kupata au kuambukiza wengine. Ni ukweli hakuna thamani yeyote kujiwela kwenye hatari”

Huo ni ujumbe wa Yarde ukiwa na hisia za masikitiko na uchungu wa kumpoteza baba yake. Ujumbe huu bila shaka utawasaidia maelfu ya watu Uingereza na duniani kwote walipota kufikiwa, wewe uliyesoma makala hii ukiwa mmoja wao. Jikinge kwa kusalia nyumbani na kuepusha safari zisizo lazima.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.