Antony Matheus Dos Santos mchezaji mpya wa klabu ya Manchester United akitokea klabu ya Ajax Amsterdam ya nchini Uholanzi leo ametambulishwa kwenye klabu yake mpya hiyo yenye maskani jijini Manchester.
Mchezaji huyo raia wa Brazil amefanikiwa kujiunga na mwalimu wake wa zamani klabuni Ajax ambaye nae pia amejiunga na United kipindi hicha cha majira ya joto.

Winga huyo hatari alieweka rekodi ya usajili nchini Uholanzi kwa kusajiliwa kwa gharama kubwa zaidi kwa kiasi cha €milioni 100 amekua na kiwango bora ndani ya klabu ya Ajax tangu ajiunge klabuni hapo akitokea Sao paulo ya kwao nchini Brazil alipodumu kwa miaka miwili.
Antony anakua mchezaji wa tano kusajiliwa klabuni hapo msimu huu na kuungana wachezaji kama Ericksen,Tyrell Malacia,Casemiro, pamoja na Lisandro Martinez.
Mchezaji huyo natazamiwa kufanya makubwa zaidi klabuni hapo na kufuta utamuduni uliokuepo wa wachezaji wanaotoka bara amerika ya kusini kutokufanya vizuri haswa nchini Brazil.

