Antony huenda asicheze kwenye mechi ya Alhamis dhidi ya Leicester lakini anaweza kucheza mechi ya kwanza dhidi ya Arsenal kwenye Uwanja wa Old Trafford Jumapili.

Masharti binafsi yamekubaliwa na kijana huyo mwenye umri wa miaka 22, kwa mkataba wa Paundi (£86M) ambaye alikamilisha vipimo vya Afya huko Carrington Jumatatu.

Antony: Man Utd Imethibitisha Makubaliano na Ajax

Antony anatakiwa kusajiliwa kwenye mfumo wa FA ili kuweza kucheza mechi dhidi ya Leicester City Alhamis. Inafikiriwa kuwa hilo haliwezekani kwani visa yake na kibali cha kufanya kazi bado havijakamilishwa.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Manchester United (@manchesterunited)

Kwa hivyo anaweza kucheza mechi yake ya kwanza na Manchester United dhidi ya Arsenal kwenye Uwanja wa Old Trafford Jumapili.

Antony: Man Utd Imethibitisha Makubaliano na Ajax

Antony ana mabao 31 na asisti 27 katika mechi 134 alizochezea Ajax na Sao Paulo, na mabao mawili na asisti mbili katika mechi tisa za Timu ya Taifa Brazil. Ameshinda mataji mawili ya Eredivisie, na medali ya dhahabu katika mechi za Olimpiki mwaka 2020.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa