MWAMUZI wa Mchezo kati ya Singida BS na Mbeya City Ahmada Simba kutoka mkoani Kagera, amefungiwa kwa kipindi cha miezi mitatu (3) baada ya kutenda kosa la kushindwa kutafsiri vyema sheria za mpira wa miguu, hasa katika tukio la adhabu ya mkwaju wa penati iliyowapatia Singida Bs bao la kwanza.

Hii ni Mara ya pili kwa Mwamuzi huyo kufungiwa ambapo mwaka 2017 Kamati ya Bodi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi za Tanzania ilimwondoa Mwamuzi wa kati, Ahmada Simba katika orodha wa waamuzi watakaochezesha mechi za Ligi Kuu kwa kipindi hicho “Ligi kuu ya Vodacom” Tanzania Bara msimu wa 2016/2017.

TPLB: Mwamuzi Simba Afungiwa Miezi (3)
Ahmada Simba Akimuonesha kadi nyekundu mchezaji wa Yanga Sc Obrey Chirwa, kwenye mechi kati ya Ruvu Shooting Vs Young Africans 2016/2017

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya utetezi wa Simba kudai kwamba hakuona tukio la Mchezaji wa Young African, Obrey Chirwa ambaye alifunga bao ambalo hata hivyo, mwamuzi alilikataa na kumwonya mchezaji kwa kadi njano ambapo baadaye alimuonya tena kadi ya pili ya njano na kumtoa nje kwa kadi nyekundu.

Katika tukio jingine, Mwamuzi wa kati aliyechezesha mchezo kati ya Coastal Union dhidi ya Yanga SC uliofanyika Agosti 20, 2022 Jijini Arusha, Raphael Ikambi kutoka mkoani Morogoro ameondolewa kwenye ratiba ya waamuzi kwa mizunguko mitatu baada ya kutenda kosa la kushindwa kutafsiri vyema sheria za mpira wa miguu.

TPLB: Mwamuzi Simba Afungiwa Miezi (3)

Ikambi alishindwa kufanya maamuzi sahihi kwa mujibu wa sheria za mpira wa miguu, katika tukio ambalo mchezaji wa Coastal Union, Mteje Albano alimchezea mchezo hatarishi na usio wa kiungwana mchezaji wa Yanga SC, Yanick Bangala ambaye baada ya tukio hilo aliinuka na kwenda kumsukuma Mtenje Albano.

TPLB: Mwamuzi Simba Afungiwa Miezi (3)

Kanuni ya 1 (a) Inahusu Nidhamu;

Kudumisha tabia njema nje ya uwanja na wakati wote wa mchezo kwa kucheza bila kuwaumiza au kuhatarisha usalama wa wachezaji wa timu pinzani”

Kutorejeshea-Kanuni ya 1(c);

“Kutorejeshea (retaliation) iwapo mchezaji atafanyiwa rafu au kukashifiwa”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa