Faini kwa Ushirikina: Tanga, Moshi na Kagera

USHIRIKINA kwenye Ligi kuu ya NBC umekuwa ukijitokeza siku hadi siku, na hii imepelekea Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kukaa kikao kujadili vitendo hivi.

Kamati hiyo ilipitia matukio mbalimbali ambayo yalijitokeza kwenye michezo iliyopita na kubaini kuwa timu za Coastal Union kutoka Tanga, Kagera Sugar kutoka Kagera, pamoja na Polisi Tanzania kutoka Moshi zilibainika kujihusisha na vitendo vya Ushirikina katika michezo yao.

Tanga, Moshi na Kagera, Faini kwa Ushirikina

Mechi namba 6 kati ya Coastal Union na KMC, ilionekana kuhusishwa na vitendo hivyo, amabpo Coastal Union imetozwa faini ya Tsh 1M, kwa kosa la baadhi ya wachezaji na maofisa wake kumwaga vitu vyenye asili ya kimiminika uwanjani wakati wakipasha moto misuli kabla ya mchezo kuanza.

Mechi namba 8 Azam FC na Kagera Sugar (2-1), mchezo huu umefanya timu ya Kagera Sugar kutozwa faini ya Tsh 1M Kwa kosa la baadhi ya wachezaji na maofisa kumwaga vitu vyenye asili ya mbegu uwanjani wakati wakipasha moto misuli kabla ya mchezo kuanza Agosti 17, 2022. Adhabu jii imezingatia kanuni ya 47:30 ya Ligi kuu kuhusu udhibiti kwa klabu.

Tanga, Moshi na Kagera, Faini kwa Ushirikina

Nao Polisi Tanzania hawakuwa nyuma kwenye kuhakikisha wanapata faini ya Tsh 1M, kwa kosa la wachezaji wake kumwaga vitu vyenye asili ya unga wakati wakiinga uwanjani kupasha moto misuli kabla ya kuanza kwa mchezo dhidi ya KMC, Agost 21, 2022 kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha. Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 2-2.

Kamati pamoja na Bodi ya Ligi imezitaka klabu kuacha mara moja imani za ushirikina kwani kufanya hivyo ni kosa na adhabu ya sasa ni kati ya faini ya Tsh 1M hadi Tsh 10M. Pia wamesisitiza kuwa vitendo hivyo vinaichafua Ligi kuu ambayo imekuwa maarufu hivi karibuni barani Afrika.

Acha ujumbe