Ushirikina Faini Mpaka Tsh 10M

Ushirikina wapigwa marufuku kwenye michezo yote ya Ligi kuu na Mpira wa Miguu kwa ujumla wake; hii ni baada ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, kukaa kikao tarehe 26 Agosti 2022.
Kamati hiyo imezitaka klabu zote kuacha mara moja vitendo vinavyoashiria imani za Ushirikina viwanjani, kwani vinachafua taswira ya Ligi Kuu ya NBC, ambayo imejizolea umaarufu mkubwa barani Afrika.

Kuonesha vitendo vya Ushirikina ni sifa mbaya, jambo ambalo linaweza kushusha hadhi ya Ligi hiyo, hivyo kamati imepanga kutoa adhabu kali kwa klabu yeyote itakayofanya vitendo hivyo kuanzia tarehe ya taarifa hii, kama kanuni ifuatayo inavyoainisha.

Ushirikina Faini Mpaka Tsh 10M

Kanuni ya 47: 30: “Timu ikifanya kitendo chochote kinachoashiria imani za ushirikina, itatozwa faini ya kati ya shilingi milioni moja (1,000,000/=) na Milioni kumi (10,000,000/=)

Aidha, kamati imezikumbusha klabu zote kutii matakwa ya kanuni ya 17:6 ya Ligi kuu, kuhusu taratibu za mchezo kama ilivyoainishwa hapa chini na kwamba, klabu yeyote itakayokwenda kinyume itaadhibiwa kwa mujinu wa kanuni.

Ushirikina Faini Mpaka Tsh 10M

 

Kanuni ya 47:30; “Timu zinazocheza mchezo husika zinatakiwa kuwasilisha kwa kamishina au Mratibu wa mchezo, orodha ya viongozi wasiozidi nane (8) na wasiopungua watano (5) na wachezaji wasiozidi ishirini (20) kwa mchezo husika masaa mawili kabla ya muda wa kuanza mchezo “kickoff” kwa kutumia fomu maalum iliyojazwa kwa unadhifu na ukamilifu ikiwa imesainiwa na kila mmoja.

Acha ujumbe