Cristian Romero beki huyu anayeitumikia klabu ya Tottenham hotspurs yenye maskani yake jijini London ameongeza mkataba wa kuitumikia klabu hiyo mpaka 2027.

Cristian Romero beki wa zamani wa Atalanta ya nchini Italia na timu ya taifa ya Argentina alijiunga na klabu hiyo kwa mkopo akitokea klabu ya Atalanta ambapo ameitumikia Spurs kwa msimu mzima kabla ya kupewa mkataba mpya na klabu hiyo siku ya leo.

CRISTIAN ROMERO

Klabu ya Spurs inapambana kuimarisha kikosi chake kwajili kushindana kubeba ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza na hii ni baada ya kufanya sajili kadhaa kikosini pamoja kuwapa mikataba rasmi wachezaji waliokua nao kikosini.

Romero amekua mhimili mkubwa katika safu ya ulinzi ya Tottenham chini ya mwalimu Antonio Conte akisaidiana na mwingireza Eric Dier na klabu hiyo kuamua kumpa mkataba wa kudumu mpaka 2027 ndani klabu hiyo.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa