Hassan Mwakinyo (27) baada ya kupoteza pambano la jana usiku kwa TKO kutoka kwa Muingereza Liam Smith, huenda tukamuona tena akirejea uwanjani kwenye marudio ya mechi hiyo ambayo ilimalizika katika raundi ya 4.
Mwakinyo ameposti kwenye mitandao ya jamii akiwa na bingwa wa dunia, James Buddy McGirt na kuandika kuwa “Rematch is on fire” kwa maana ya kwamba marudio ya pambano lake liko mbioni kurudiwa.
Bondia huyo ambaye alianza vizuri kwenye raundi ya kwanza akionekana kuutawala mchezo zaidi, kwa kumpelekea makonde Liam sehemu mbalimbali ya mwili wake kama vile kichwani, na tumboni, Hassan alipata na hitilafu ya mguu na hivyo kusababisha kutokuendelea kwa pambano hilo.
View this post on Instagram
Akielezea changamoto alizokutana nazo kabla ya pambano lake, alisema moja ya sababu iliyochangia kupoteza pambano kwa TKO ni kupotelewa na begi lenye vifaa vyake vya kupigania kitu ambacho alikiita kama ni “hujuma”
Mpaka sasa bondia huyo ana jumla ya mapambano 20 aliyoshinda akiwa kashinda kwa KO’s mara 18 na kupoteza mapambana matatu ukijumlisha na lile la jana dhidi ya Liam Smith.