Kocha mkuu wa klabu ya Manchester United Erick Ten Hag amesema kuwa anapanga kuwa mwalimu na rafiki wa Cristiano Ronaldo msimu huu, baada ya kuwa na maelewano mabaya na klabu hiyo toka msimu huu uanze.

Nyota huyo wa Kireno alibaki pale Old Traford licha ya kuripotiwa anataka kuondoka katika dirisha hili la usajili baada ya timu yake kushindwa kufuzu katika michuano mikubwa barani Ulaya (UEFA). Alikuwa akihusishwa kwenda Napoli ambayo kwa sasa ipo kwenye ubora wake pale Serie A.
Tetesi zilivuma sana hadi siku ya mwisho ya dirisha la usajili lakini, Ronaldo aliyerejea katika kikosi hico akitokea Juventus msimu uliopita alikuwa ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa kwenye kikosi kichokuwa kinaenda kuvaana na Leicester City, huku akitokea benchi mchezo ambao uliomalizika kwa United kushinda kwa bao 1-0.
Ten Hag anaongezea kwa kusema kuwa Ronaldo alibaki kama tulivyosema kwani ni mapema sana, na tuna wachezaji wengi wa kuanza katika kikosi cha kwanza cha wachezaji 11 na ndivyo ambavyo inatokea sasa. Anasema,

“Wachezaji ambao wapo benchi wanaweza kucheza ndani ya wiki moja, mbili, au tatu”
Ten Hag aliendelea kwa kusema Ronaldo aliingia na kucheza kwenye mchezo dhidi ya Brentford ambapo aliingia uwanjani kwa aibu kubwa kwani walikuwa wameshapwa mabao 4-0, na tokea siku hiyo wapokee kichapo hicho cha aibu kutoka kwa Brentford ndipo walikuja kushinda mechi zao dhidi ya Liverpool, Southampton pamoja na ushindi walioupata kwa Leicester City.
Ameeleza pia sababu za Ronaldo kukosa nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza ni sababu kuwa Ronaldo amekosa mechi nyingi za maandalizi ya msimu huu, kutokana na matatizo ya kifamilia. Huku mabosi wa timu hiyo wakisema Ronaldo atachukuliwa sawa kama wachezaji wengine wanavyochukuliwa kutokana na hali itakayokuwepo.

