Klabu ya Namungo siku kadhaaa zilizopita walitangaza Kumuaga rasmi kiungo Mshambuliaji Mohammed Issa Banka lakini Leo wametangaza usajili mpya wa Mkongwe Frank Domayo Chumvi.

Namungo wameongeza kiungo mwingine Mwenye uwezo mkubwa wa Kupiga Pasi Kwenye Njia na kurahisisha Kazi ya Washambuliaji kupachika mabao naye si mwingine bali ni Frank Domayo.
Domayo kafanya hiyo kazi katika misimu kadhaaa Kwani tayari ameshafanya akiwa Yanga na Azam na hata timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars anaenda kuungana na Lukasi kikoti ,Jacob Massawe ambao wamekuwa na mchango mkubwa kwa Namungo kupata matokeo ya Ushindi.

Namungo wnaendelea ma mazoezi kwaajili ya mchezo wao unaofuata wa Ligi kuu ambapo watasafiri hadi Tanga kumenyana dhidi ya Wagosi wa Kaya Coastal Union.

